Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda akiwa mkoani Manyara kwa lengo la Kuwashukuru na kuwasikikiza Walipakodi amefanya mkutano na Wafanyabiashara na kueleza kuwa TRA itaendelea kutatua changamoto za Walipakodi kwa njia ya mazungumzo.

Amesema jukumu la TRA ni kuona Biashara nchini zinakuwa hivyo panapokuwa na vikwazo wamekuwa wakiviondoa ili kuboresha Mazingira ya biashara na kuwawezesha kukusanya kodi.

“Kipaumbele chetu ni biashara halafu Kodi inafuata maana huwezi kukusanya Kodi pasipo kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia biashara wafanyabiasha” amesema Bw. Yusuph Mwenda

Kamishna Mkuu Mwenda ameeleza kuwa kwa Mwezi December TRA imekuwa ikitoa shukrani kwa Walipakodi na kuwasikiliza utaratibu ambao umewezesha kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili Walipakodi na kukosa utatuzi wake.

Katika ziara hiyo mkoani Manyara Kamishna Mkuu Mwenda amekabidhi zawadi kwa baadhi ya walipakodi akiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya Twiga General Traders Ltd Bw. Richard Ngalewa ambaye amejipambanua kama mlipakodi anayetoa elimu ya mlipakodi kwa wengine.

“Huyu ni Mlipakodi wa kipekee aliyejipambanua kama mtoa elimu ya Kodi kwa Walipakodi wengine mkoani Manyara hususan hapa kwenye mji wa Babati hivyo kama Mamlaka tunawajibika kumtambua na kumshukuru kwa kuwa balozi wetu mzuri” Amesema Bw. Mwenda.

Akizungumza baada ya kupatiwa zawadi Bw. Richard Ngalewa amesema anaendelea kutoa elimu kwa walipakodi wengine ili kuongeza idadi ya walipakodi.

Mfanyabiashara huyo ameuomba uongozi wa TRA kuangalia namna bora ya kutoza kidi ya ongezeko la thamani (VAT) ili kuleta usawa na ushindani sokoni jambo ambalo Kamishna Mkuu wa TRA ameahifi kulifanyia kazi.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda cha MATI kinachozalisha Pombe Kali maarufu kama Vinywaji changamshi Bw. David Mulokozi amesema wataendeleza ubora na kusimamia sheria za TRA katika ulipaji wa kodi.

Katika mkutano wa wafanyabiasha na Kamishna Mkuu wa TRA, Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Jitu Soni ameitaka TRA kuitazama sekta ya kilimo katika masuala ya Kodi hasa kwenye pembejeo.

Amesema ndani ya nchi wapo wazalishaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo Mipira ya umwagiliaji ambao wamekuwa wakitozwa Kodi lakini vifaa vya umwagiliaji kutoka nje ya nchi vimekuwa vikiingizwa bila kutozwa kodi jambo ambalo linadhoofisha viwanda vya ndani.

Naye Katibu wa Umoja wa wafanyabiasha mkoa wa Manyara (TCCIA) Bi. Zaynab Sadiki ameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuishauri Serikali iondoe sheria za kodi zilizopitwa na wakati ili kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara.

Amesema katika mkoa wa Manyara wamekuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiasha wenzao pamoja na Uongozi wa TRA ili kujadili na kutatua kwa pamoja changamoto zinazowakabili.

Kamishna Mkuu wa TRA ameahidi kufanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na wafanyabiasha mkoani Manyara. 

About Author

Bongo News

1 Comment

    I will immediately seize your rss as I can’t find your e-mail subscription hyperlink or newsletter service. Do you’ve any? Please let me know so that I could subscribe. Thanks.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *