Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, ameitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria na kanuni zinazosimamia biashara ya madini ya Tanzanite, akisisitiza kuwa zuio la kuuza madini hayo nje ya eneo la Mererani linachangia hasara kubwa kwa taifa.

Gambo ameyasema hayo Ijumaa, Oktoba 18, 2024, wakati wa mkutano na wafanyabiashara wa madini na ma-brokers uliofanyika katika Soko la Madini, mkoani Arusha.

Akizungumza kuhusu namna ambavyo sera za sasa zinaathiri sekta ya madini, Gambo amefafanua kuwa katika miaka ya nyuma, thamani ya madini ya Tanzanite ilikuwa juu, ikifikia hadi dola 2000 kwa gramu, lakini kutokana na maamuzi yasiyo sahihi na ubinafsi, thamani hiyo imekuwa ikishuka siku baada ya siku.

“Taifa linapata hasara, nchi inapata hasara kwa sababu ya ubinafsi. Unailinda Mererani, unaliua taifa,” amesema.

Gambo pia ameeleza kwamba licha ya kuwa Mererani ndiyo eneo pekee la kuchimba Tanzanite, serikali haipaswi kuzuia madini hayo kuuzwa sehemu zingine ndani ya nchi. Alilalamika kuwa kwa sasa ni rahisi kupeleka madini hayo nje ya nchi, kama vile India na Marekani kuliko kuyapeleka katika miji ya Tanzania kama Arusha au Dar es Salaam.

“Leo ukienda Mererani na ukinunua madini yako, ukilipa mrabaha, unaruhusiwa kuyapeleka India, Marekani, Dubai, Kenya, lakini huruhusiwi kuleta Arusha au Dar es Salaam,” amesisitiza Gambo.

Leo Arusha inajivunia kuuza mchanga na kokoto, na siyo madini ya Tanzanite tena. Hiyo si habari njema. Mapato yameshuka, na ukienda kwenye utafiti uliofanywa na Wizara ya Madini yenyewe, moja ya sababu ya kushuka kwa madini ni zuio la kutaka madini yawe Mererani peke yake,” amesema Gambo.

About Author

Bongo News

2 Comments

    Üsküdar su kaçağı problemleri Rothenberger cihazı ile su kaçağı tespit edildi, Üsküdar’daki evimde hiçbir yeri kırmadan sorun çözüldü. https://socialhustle.co.uk/read-blog/9615

    Keep up the fantastic work! Kalorifer Sobası odun, kömür, pelet gibi yakıtlarla çalışan ve ısıtma işlevi gören bir soba türüdür. Kalorifer Sobası içindeki yakıtın yanmasıyla oluşan ısıyı doğrudan çevresine yayar ve aynı zamanda suyun ısınmasını sağlar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *