KITAIFA

UCHUNGUZI UFANYIKE KUZUKA KWA MOTO BONDE LA MZAKWE

UCHUNGUZI UFANYIKE KUZUKA KWA MOTO BONDE LA MZAKWE

Pichani ni sehemu ya eneo lililoathirika na moto katika bonde la Mzakwe, chanzo
cha moto huo bado hakijajulikana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameviagiza vyombo
vya ulinzi na usalama Mkoani Dodoma kuhakikisha vinawasaka na kuwabaini
wote waliohusika na uchomaji moto katika bonde la mzakwe hii.
Senyamule ametoa agizo hilo Julai 21, 2023 mara baada ya kufika katika
eneo hilo kujionea athari za uharibifu zilizosababishwa na moto ulioanza
majira ya saa saba mchana.

Amesema asilimia 70 ya maji katika Jiji la Dodoma yanatoka katika bonde la
Mzakwe na ni eneo la hifadhi hivyo ni muhumimu kukakikisha linalindwa na
kuhifadhiwa kwa ustawi wa afya na mazingira ya watu wote.
Aidha, amewapongeza vijana wa JKT Makutupora walioshiriki katika zoezi la
kuzima moto uliotokea katika Bonde la Mzakwe Jijini Dodoma. Senyamule
amewapongeza kwa uzalendo walionyesha wa kudhibiti moto huo na kuzuia
madhara makubwa ambayo yangeweza kujitokeza, amesema wameonyesha
uzalendo mkubwa, uhodari na ushupavu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipata maelezo ya awali kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Julishaeli Mfinanga kuhusu moto ulioteketeza eneo la bonde la Mzakwe Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu


“Tumesikitishwa sana na moto huu kwa kuwa si kwamba umeathiri ikolojia ya
eneo hili lakini pia umeharibu miundombinu ya Tanesco ikiwa ni pamoja na
nguzo, hivyo kwanza nawapongeza vijana wetu kwa jitihada za kufanikisha
kuzima moto huu na pili vyombo vyote vinavyohusika na uchunguzi vifanye
kazi yake ili kubaini chanzo” Senyamule amesisitiza.
Aidha Senyamule amemuagiza Meneja wa Bonde la Wami Ruvu kuhakikisha
kuwa wanachonga barabara maalumu kwa lengo la kukinga moto katika
bonde hilo ili athari za moto zisiwe kubwa pindi moto utokeapo.
Awali Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Dodoma Julishaeli
Mfinanga amesema kuwa walipata taarifa kwa njia ya simu kupitia namba za
dharura 114 na kuwahi eneo la tukio kwa haraka. Amesema moto
umedhibitiwa na hakuna madhara makubwa na wanaendelea na doria
kuhakikisha usalama katika eneo lote la bonde.

About Author

Bongo News

1521 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *