*Taa kuangaza barabara kuelekea Kusini

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza kuwa serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 114 kukarabati barabara za mikoa ya Kusini zilizoharibiwa na mvua za El Nino huku akiagiza taa za kutosha kuwekwa kwenye barabara kuu kuelekea mikoa ya Kusini.

Akizungumza katika maeneo tofauti wakati wa ziara yake mkoani Lindi jana na leo, Ulega alisema kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa mkoa wa Lindi ndiyo kikubwa zaidi kutengwa kuliko mkoa mwingine wowote hapa nchini.

“ Ndugu zangu wa Lindi, nimekuja kukagua barabara zetu baada ya matatizo ya mvua za El Nino na hiki kimbunga cha Hidaya. Rais ameniagiza nije huku kuangalia hali na kuwapa pole kwa changamoto mnazopitia.

“Kwa mapenzi yake makubwa kwenu na kwa Watanzania kwa ujumla wake, Rais Samia ameagiza tutumie zaidi ya shilingi bilioni 114 kwa ajili ya kurekebisha barabara na madaraja yaliyoharibiwa na kutengengeza njia za kuchepusha, “ alisema Ulega wakati akiwa eneo la Somanga.

Mvua za El Nino zilizonyesha nchini mwishoni mwa mwaka jana zilifuatia msimu wa mvua za masika zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo tofauti nchini, ingawa mikoa ya Kusini iliathirika zaidi.

Katika ziara yake hiyo, Ulega alijionea mwenyewe uharibifu uliosababishwa na mvua hizo na pia juhudi za wakandarasi wanaojenga barabara hizo – wakiwamo wakandarasi wazalendo.
Katika hatua nyingine, Ulega ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuanza kuweka taa katika barabara kuu inayoelekea mikoa ya Kusini ili kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo inakopita.

Waziri huyo ambaye sasa ameanza kujipambanua kwa kauli mbiu yake ya Usiku na Mchana, alisema sera za Rais Samia ni za kukuza uchumi na kuwa maeneo ambako kuna giza ni vigumu kwa uchumi kukua.
“TANROADS naomba taa zianze kuwaka kwenye barabara hii ya kuja Kusini mwa Tanzania. Haya ni maelekezo ya Rais wetu na kazi yenu ni kuhakikisha mnatekeleza agizo hilo kwa kufanya kazi usiku na mchana,” alisema.

Mbali na kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu, Ulega pia anatumia ziara hii kueleza mafanikio kadhaa yaliyopatikana kwenye eneo la ujenzi kwenye miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia.

About Author

Bongo News

4 Comments

    I don’t even know how I ended up here, but I thought
    this post was great. I do not know who you are but certainly you’re going to a famous blogger if
    you are not already 😉 Cheers!

    If you desire to grow your knowledge only keep visiting
    this site and be updated with the most recent gossip posted here.

    This paragraph provides clear idea designed for the new visitors of blogging, that really how to do blogging.

    I’m gone to convey my little brother, that he should also
    pay a visit this blog on regular basis to obtain updated
    from latest gossip.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *