Umoja wa Mataifa (UN) umeunga Mkono kile kinachofanywa na Kampeni ya Mama Samia Legal Aid ( #MSLAC )ambayo imekuwa ikitoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa Wananchi.

Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Ester Msambazi amesema imekuwa ni faraja sana kwa Serikali kwamba kinachofanyika kwenye kampeni hiyo hata umoja wa Mataifa umekiona na kukithamini kwamba kinafikia Wananchi walengwa.

Ameyaeleza hayo jana tarehe 9 Julai 2024; kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria lililopo kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba Temeke Jijini Dar- es Salaam.

Amesisitiza “nimeona sasa tunaenda kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na kampeni itakimbia sana kwa sababu wao kuonesha wamethamini kampeni yetu, inamaana kubwa saana kwetu kwamba sasa tutakwenda kupata wadau wengi zaidi Umoja wa Mataifa UN watatuunga Mkono na tutafikia Wananchi kwa kiasi kikubwa kwa sababu masuala ya huduma kwa jamii, msaada wa kisheria sio suala la Serikali pekee yake’

Baadhi ya Wananchi wanufaika wa huduma hiyo wamesema kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa hasa kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya kisheria ambao hawajui waanzie wapi. MSLAC

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *