Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo mkoani Pwani watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya jirani.
Upimaji huo utafanyika siku ya Jumatano tarehe 19/07/2023 saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0716633913 Dkt. Kandy Lussingu Mkuu wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, 0759328117 Dkt. Luiyana Lyimo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Bagamoyo na 0733860575 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Bagamoyo.
1 Comment
JP-Dolls.comは、リアルドール市場において非常に高い評価を得ているオンラインショップです.セックス ドール