Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Tanzania bara Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amesema kutekelezwa kwa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa pande zote mbili za Muungano ni alama muhimu katika ushirikiano wa Wizara za Katiba na sheria ya Bara na Visiwani, akihimiza mashirikiano hayo kuwa na tija na maslahikatika kunufaisha zaidi wananchi kupitia Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria.

Akizungumza wakati akitoa salamu za Wizara visiwani Zanzibar kwenye Viwanja vya Tumaini Skuli ya Mkwajuni leo Aprili 23, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo amesema kwamba katika kuimarisha mahusiano ya Wizara hizo, ipo mikakati na programu wanazoshirikiana ikiwemo kubadilishana teknolojia na uzoefu kwa wataalamu wa Wizara hizo, kushughulikia kesi za uhujumu uchumi na udhalilishaji kwa pamoja na mashirikiano katika Mkakati wa utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia.

Katika hatua nyingine Dkt. Rwezimula amebainisha kuwa tangu kuzinduliwa kwa Kampeni hiyo miaka miwili iliyopita, mwitikio umekuwa ni mkubwa kwa wahitaji mbalimbali upande wa Tanzania bara ambapo changamoto mbalimbali za kisheria zimetatuliwa, uelewa wa jamii kuhusu masuala ya sheria umeimarika pamoja na wananchi wengi wanyonge kupata uwakilishi wa Mawakili kwenye mahakama za ngazi mbalimbali nchini.

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Rwezimula kadhalika ametumia sehemu ya hotuba yake kumpongeza mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, utumishi na utawala bora Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman kwa uwajibikaji wake katika kustawisha ustawi wa haki na utawala bora Visiwani Zanzibar sambamba na mashirikiano mazuri ya Wizara yake na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *