Mwaka 1967 Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere aliongoza matembezi kuanzia kijijini kwao Butiama kwenda Mwanza mjini kuunga mkono matokeo ya Azimio la Arusha.
Baada ya miaka 57, leo Oktoba 9, 2024 Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) tumeanzia pale alipopita Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kutembea zaidi ya kilometa 200 kuenzi miaka 25 ya tangu alipotutoka na matembezi yatapokelewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mkoani Mwanza.
Matembezi yamezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Cde. Rehema Sombi (MNEC) kwenye Uwanja wa CCM wilayani Butiama akiambatana na Katibu Mkuu, Cde. Jokate Mwegelo ambapo vijana zaidi ya 2,000 watatembea kwenda mkoani Mwanza na njiani watakuwa wakihamasisha ushiriki wa vijana kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Wiki ya Vijana.
1 Comment
Tempat paling asik bermain slot game hanya di big77