KITAIFA

VIUATILIFU NA MBOLEA VITUMIKE KWA KIWANGO MAALUM

VIUATILIFU NA MBOLEA VITUMIKE KWA KIWANGO MAALUM

Zikiwa zimebaki siku 3 kuelekea kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Wizara ya Kilimo imeeleza umuhimu wa utafiti katika kufanya kilimo cha kisasa, chenye tija na manufaa makubwa kwa wakulima

Wizara hiyo imeweka bayana kuwa utafiti umeendelea kuwezesha upatikani wa mbegu Bora za mazao zenye sifa za kustahimili mabadiliko ya tabia nchi, kuhimili ukame, magonjwa na wadudu waharibifu huku mavuno yakiwa yanaongezeka mara dufu.

Aidha, Ili kuongeza tija ya mavuno kwa Wakulima, Watafiti wamegundua hatua mbalimbali za kupanda mazao mbalimbali badala ya kupanda kiholela bila kuzingatia vipimo mfano Katika zao la Pamba upandaji wa sentimita 60 mstari hadi mstari na sentimita 30 shimo hadi shimo limewaongezea wakulima tija kulinganisha na hatua za awali za sentimita 90 kwa 40.

Vilevile, katika Upandaji wa sentimita 60 kwa sentimita 30 inaongeza wingi wa mimea kufikia 44,444 Kutoka 22,222 Katika upandaji wa zamani hatua ambayo inapelekea ongezeko la mazao.

Wizara imeeleza kuwa Matumizi ya viuatilifu na pembejeo za mbolea ni muhimu, lakini kwa Kiwango maalumu kwa kuzingatia sababu mbalimbali Watafiti wameendelea kutafiti na kushauri viwango maalumu vya mbolea vinavyofaa kutumiwa katika mazao na mbegu husika Katika maeneo waliopo.

Suala la afya ya Udongo ni muhimu Katika Kilimo hivyo tafiti zimekuwa zikifanyika kuhakikisha mkulima analima kwa tija kwa kuzingatia hilo Miongoni mwa matokeo ni Utafiti uliobaini uchachu Katika udongo na Watafiti wanashauri matumizi ya chokaa Kilimo kwa kuzingatia hali ya eneo husika kadri ya ushauri wa wataalamu unavyotolewa Kutoka na Kiwango cha athari iliyopo.

Kwa upande wa uongezeaji thamani mazao, Utafiti umesaidia kupunguza hasara anayopata Mkulima na hatimaye kumuongezea tija mfano zao la zabibu sio tu kutafuna bali inatumika pia kutengeneza bidhaa zingine ikiwemo mvinyo, zabibu za mezani na viungo hivyohivyo korosho na mazao mengine Watafiti wanatoa elimu ya uongezaji thamani ambayo imewezesha kupunguza hasara kwa Mkulima.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *