Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanzisha Ofisi ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu hali ambayo itaongeza ufanisi katika kuhudumia kundi hilo ambalo ni wachangiaji wakubwa wa mapato ya TRA.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu kwa nyakati tofauti Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wamepongeza ubunifu uliofanywa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda kwa kuanzisha Ofisi hiyo ambayo ina hadhi inayotakiwa.

“Ubuni huu ni wa kipekee kabisa na unaweza usiamini kama Serikali inaweza kuwa na Ofisi zenye hadhi kiasi hiki, hata Walipa Kodi wenye hadhi ya juu wakija kuhudumiwa wataona wamethaminiwa” wamesema baadhi ya Wabunge wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Oran Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wakithaminiwa hata mapato ya TRA yataongezeka zaidi maana watalipa Kodi kwa hiari na kujenga urafiki na TRA.

Mhe. Njeza amesema Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu wanapopewa hadhi wanayostahili wanajisikia kuwa kulipa Kodi ni haki yao maana wanapata huduma zinazowastajili.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Mwenda amesema lengo la kuanzisha Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ni kutaka kuwapa huduma inayolingana na hadhi yao.

Amesema Ofisi hiyo ya Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ina watumishi wabobezi katika masuala ya Kodi na huduma kwa wateja, huku kukiwa na mazingira mazuri ya kutolea huduma yenye hadhi ya juu.

Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema ili kuboresha huduma za Walipa Kodi binafsi wenye hadhi ya juu ameanzisha utaratibu wa kuwafuata Walipa Kodi hao na kuzungumza nao.

About Author

Bongo News

1 Comment

    This is very attention-grabbing, You are a very skilled blogger.
    I’ve joined your rss feed and stay up for in the hunt for extra of your magnificent post.
    Also, I’ve shared your website in my social networks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *