BIASHARA

WANANCHI MIRERANI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUTOA FURSA KWA WAWEKEZAJI WAZAWA KUWEKEZA KWENYE VITALU

WANANCHI MIRERANI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUTOA FURSA KWA WAWEKEZAJI WAZAWA KUWEKEZA KWENYE VITALU

Wafanyakazi wa Kampuni ya wawekezaji wazawa Franone Mining and Games Campany LTD,inayochimba Madini ya Tanzanite eneo la Kitalu C,Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.Samia Suluhu Hassan kwani wameweza kupata ajira tofauti na ilivyokuwa awali.

Wakizungumza kwenye mgodi huo hivi karibuni walimshukuru mwekezaji huyo kwa kuwapatia ajira ambapo huko nyuma hawakuwa na kazi ya kufanya kwa ajili ya kuwapatia kipato lakini sasa hivi wamekuwa na uhakika wakujipatia kipato kinachotokana na hiyo kazi.

kwa upande wake Nai leyani ambaye ni kiongozi wa kikundi cha akina mama wanaofanya kazi katika kampuni hiyo amesema serikali iendelee kumlinda mwekezaji huyu na kuwapa elimu wachimbaji wadogo ili kuondokana na tatizo la mitobozano ambayo imekuwa ni kero kwa mwekezaji kwa sababu wapo watu wanaoamini kuwa kitalu C peke yake ndiyo kinamadini.

Alisema pasipo serikali kuangalia kwa jicho tatu mwekezaji hatoweza kuendelea na shughuli kwa sababu wachimbaji wadogo wanadaiwa kuendelea kuchimba kuelekea kwenye kitovu cha Kitalu c,”alisema Nai.

Naye Joram Madole mwakilishi wa Wazee walionufaika na uwekezaji huo amesema awali wakatika wa mwekezaji Mzungu walikuwa hawawezi kuingia kufanyakazi lakini sasa hivi wanafanyakazi kwa amani na utulivu na wanajipatia kipato cha kuwasomeshea wajukuu zao.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo,Vitus Ndakize alisema kampuni hiyo imeweza kutoa ajira rasmi 386 na ajira 1000 ambazo siyo rasmi ambao ni wachekechaji na kazi yao kubwa ni kuchekecha udongo ambao unatoka chini ya mgodi na kwa kufanya hivyo wanajipatia riziki zao.

Alisema kupitia mgodi huo wameendalea kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kuchangia michango mbalimbali ikiwemo ukarabati wa Barabara kiwango cha changalawe kutoka getini hadi mgodini hapo.

Pia aliongeza kuwa walitoa chakula katika shule mbili za Sekondari ambazo ni Mirerani, na Naisinyai kwa sababu kulikuwa na ukosefu wa mvua uliopelekea shule hizo kukosa chakula hivyo waliguswa na waliweza kutoa chakula cha mwaka mzima na kutoa madawati 100 katika shule ya Mirerani.
Katika hatua nyingine,Vitus Ndakize alisema Mgodi huo umekuwa na changamoto kubwa ya mitobozano kutokana na uelewa mdogo wa wachimbaji wadogo.

Aliongeza kuwa mikondo ya Tanzanite imelala kuanzia Kitalu A,B inapita Kitalu C na inaenda D mpaka D Extensioni na huko kote madini yapo na huo ndiyo uelekeo wa madini hayo.

Watu wengi wanaamini kuwa madini yapo kitalu C na si kwamba yapo kitalu C peke yake ni kwa sababu kitalu kilifanyiwa tafiti za kutosha hivyo kinaweza kuwa na uzalishaji endelevu kwa sababu hivyo vitalu vingine havina tafiti za kutosha kwa maana hiyo watu wanachimba kwa kubahatisha,alisema Vitus Ndakize .

Aliongeza kupitia mitobozano inaweza ikaleta maafa makubwa kwa kuuwa watu kwa sababu kule chini kazi za ulipuaji zinapofanyika na kinachofanya kazi ni baruti na inapotokea kuna mtu anaripua pasipo kuwa na taarifa watu wanaweza kujeruhiwa.

Alisisitiza ili kumaliza tatizo la mitobozano Serikali lazima iendelee kutoa elimu ya mipaka ya maeneo yao kwa sababu
wapo baadhi ya wachimbaji bado wanaamini chini ya ardhi hakuna mipaka jambo ambalo siyo kweli.

About Author

Bongo News

15 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *