KITAIFA

WANANCHI WA GALIGALI WAMSHUKURU WAZIRI SIMBACHAWENE KWA UJENZI WA BARABARA

WANANCHI WA GALIGALI WAMSHUKURU WAZIRI SIMBACHAWENE KWA UJENZI WA BARABARA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wananchi wa Kata ya  Galigali,  ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe 

Wananchi wa Kata ya Galigali iliyopo Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wamemshukuru   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene  kwa ujenzi wa barabara kwa gharama ya kiasi Shilingi Bil 1.4 kwa kumwaga zege katika maeneo korofi

Pia, Wananchi hao wamemshukuru Waziri huyo kwa ujenzi wa madaraja matatu ambayo tangu kukamilika kwake yamewarahisisha mawasiliano kwa kuunganisha  Kata hiyo na Kata zingine.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akikagua Shule ya Sekondari GaliGali ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe 

Shukrani hizo zimetolewa leo na Wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti kupitia mikutano ya hadhara ya Waziri huyo anayoendelea kuifanya katika Kata hiyo ya Galigali inayoundwa na Vijiji viwili ambavyo ni Galigali na Matonya,  ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika jimbo hilo.

Imeelezwa kuwa Kata hiyo kabla ya kukamilika kwa Barabara hiyo kulikuwa hakuna Barabara kabisa ya kuunganisha Kata moja hadi nyingine.

Wamesema imekuwa ni msaada mkubwa tangu barabara hiyo ilipokamilika  kwani ilikuwa tishio kwa Watumiaji  kabla ya kujengwa kwake kutokana na  jiografia ya Kata ambayo ipo juu milimani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akimtambulisha mke wake  wakati mkutano wa hadhara katika Kata ya Lumuma  ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe

” Kipindi cha masika tulikuwa hatuwezi kusafiri kutoka hapa kwenda Kibakwe Mjini ila kwa sasa tunaweza kusafiri kwani sehemu zote korofi zimeimarishwa kwa kuwekewa zege, Tunamshuru sana Mbunge wetu, amesema Onesmo Mwanchali Mkazi wa Kata hiyo

Wamefafanua kuwa licha ya mawasiliano ya barabara kuimarika kwa sasa ila changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa Kata hiyo kwa sasa ni kukosekana kwa mawasiliano ya simu na umeme

Wametumia fursa hiyo kumueleza Waziri kuwa  mambo mengi yamekuwa yakikwama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya simu na hivyo wamemuomba  ashirikiane  na makampuni ya simu kutatua changamoto hiyo.

Aidha, Wananchi hao wamemuomba Mhe.Simbachawene kupatiwa umeme kwa ajili ya kuchochea  maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wamesema Kitendo cha kukosa umeme katika Kata hiyo  wamekuwa wakilazimika kutumia vibatari na kulazimika kulala mapema kutokana na giza 

” Mhe.Mbunge tunatambua mchango wako mkubwa wa maendeleo katika Kata hii changa, Tunakuomba utupambanie huko tupate umeme na mawasiliano ya simu ili na sisi tuweze kuboresha maisha kama ilivyo kwa wenzetu Amesema Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mwachayeka Mussa

Akijibu changamoto hiyo ya umeme na mawasiliano, Waziri Simbachawene amesema suala la umeme atahakikisha ndani ya mwaka huu Kata hiyo inapatiwa na umeme kwani tayari ipo kwenye mpango 

Ameongeza kuwa ujio wa umeme huo utaongeza tija hivyo wananchi wa Kata hiyo wanapaswa  kufanya kazi kwa bidii ili pindi  umeme huo utakapofika waweze kumudu gharama za kuulipia ili kuingiza majumbani mwao

Kuhusu Mawasiliano ya Simu, Waziri Simbachawene ameahidi kufanya mawasiliano na Makampuni ya simu ikiwemo  Mtandao wa Airtel ili waje kuweka mnarav wao kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano.

Aidha Mhe. Simbachawene ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuubali kutoa fedha kwa ajili ya shule ya Sekondari Galigali pamoja na Barabara hiyo.

About Author

Bongo News

1 Comment

    I’m also commenting to let you understand of the amazing experience my friend’s daughter experienced reading through your webblog. She came to understand a good number of issues, including what it is like to possess an amazing helping style to have many people with no trouble learn a number of complex topics. You actually did more than people’s desires. I appreciate you for delivering the valuable, dependable, edifying and in addition unique thoughts on this topic to Gloria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *