KITAIFA

WANANCHI WA MPITIMBI B WAPEWA RAI, KUWEKEZA MABWAWA YA SAMAKI

WANANCHI WA MPITIMBI B WAPEWA RAI, KUWEKEZA MABWAWA YA SAMAKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akitembelea eneo la mradi ili kujionea hatua za ujenzi wa eneo la Mradi wa Shamba Darasa la Ukuzaji wa Viumbe Maji katika kijiji cha Mptimbi B.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ameshauri watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea kuanza kutenga maeneo yatakayosaidia wananchi kujishughulisha na utengenezaji wa Mabwawa ya ufugaji wa samaki ambayo yatachochea uchumi na kuongeza wigo wa mapato kwa Halmashauri.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akizungumza na Wananchi katika eneo la Mradi wa Shamba Darasa la Ukuzaji wa Viumbe Maji katika kijiji cha Mptimbi B.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea kujionea Mradi wa Shamba Darasa la Ukuzaji wa Viumbe Maji unaoendelea kujengwa na serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Kata Mpitimbi Halmashauri ya wilaya ya Songea leo tarehe 14/07/2023.

Waziri Mhagama ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa shamba la darasa la ukuzaji wa viumbe hai, amesema tunaweza kutumia mabwawa ya ufugaji wa samaki kama chanzo cha ajira na uchumi kwa wananchi wa Mpitimbi B.

“Mhe. Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan anamaono ya mbali sana, ametupatia mradi ambao utasaidia kuzalisha mbegu na mafunzo, tunatakiwa tuanze kujiandaa kwa kutengeneza mabwawa”.

Mhandisi Msimamizi wa Mradi, kutoka Halmashauri ya Songea Bi,Flora Tairo akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Shamba Darasa la Ukuzaji wa Viumbe Maji katika kijiji cha Mptimbi B.

Amefafanua mradi utakapokamilika; wananchi wawe na miundo mbinu yao ya mabwawa ya ufugaji wa samaki tayari, ili mafunzo yatakapokuwa yanafanyika wawe wanachukua vifaranga na kuweka kwenye mabwawa yao, alisema Waziri Mhagama.

Tunaweza tukatumia mikopo ya Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kuweza kutengeneza mabwawa yao ya ufugaji wa samaki, alisisitiza.

“tunapaswa tuwe na mabwawa Mengi ya samaki kushoto na kulia mwa eneo la mradi yatakayomilikiwa na vijana wakinamama na wazee ambayo samaki watafugwa kisasa na watakuwa na uzito mzuri alisema,” Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema Halmashauri inaanda andiko la kimkakati kwa ajili ya kupata fedha ya kuendeleza Lambo kubwa la maji lilopo katika kijiji cha Mpitimbi B ambalo linahitaji fedha Zaidi ya million 500.

Amefafanua kwamba ujenzi wa lambo hilo utaenda sambamba na Halmashauri kutaratibu kupitia Halmashauri ya kijiji maeneo ambayo wananchi watajenga mabwawa ya kufugia samaki, alisema

Awali katika taarifa Mhandisi Msimamizi wa Mradi, kutoka Halmashauri ya Songea Bi,Flora Tairo alisema Mradi uko katika hatua ya ukamilishwaji, kwa majengo na upandaji nyasi kwenye kingo za mabwawa.

Ameongeza kusema mradi utakapokamilika utakuwa na mabwawa manne, uzio, darasa la mafunzo, stoo pamoja na maliwato.

Akieleza umuhimu wa mradi Bi, Agatha Mapunda Mkazi wa Mpitimbi B amesema wanamshukuru Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi na wamejiandaa kupokea mafunzo

Amesema mradi utawasaidia kupata lishe bora na fursa za biashara zitakazojitokeza wakati wa uzalishaji.

About Author

Bongo News

1 Comment

    Транснациональные перевозки играет ключевую роль в налаживании цепочек поставок в Российскую Федерацию. Это комплексный подход, включающий перевозку грузов, обработку документов и управление цепочками поставок. Грамотная стратегия и сотрудничество с профессионалами минимизируют риски и гарантируют своевременную доставку.

    Одной из важнейших целей в грузоперевозках является определение маршрута – https://ved-mezhdunarodnaya-logistika.ru/ . Для импорта в страну используются альтернативные подходы: морские перевозки экономически эффективны, авиатранспортировка — товаров с ограниченным сроком, а поездные перевозки — в сочетании цены и скорости. Стратегическое положение часто предполагает мультимодальные подходы.

    Не менее значимым процессом является оформление документов. Грамотная обработка договорным актам, учет нормативных требований и учет санкционных ограничений обеспечивают успех. Сотрудничество с экспертами исключает ошибки, что критично для результата.

    Современные технологии существенно влияют на международную логистику. Платформы контроля, управленческие платформы и системы прогнозирования способствуют оптимизацию процессов. Это позволяет бизнесу сохранять устойчивость, учитывать новые условия и обеспечивать поставки.

    Импортные маршруты нуждается в координации, надежности команд и подбора связей. Это основной ресурс, позволяющий российским предприятиям внедрять инновации и интегрироваться в мировую экономику.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *