Waziri wa Nchi OR-MU na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo akiwa ziarani katika Kata ya Mburahati amesema barabara ya Barafu – Darajani inayounganisha wakazi wa Mburahati na Magomeni itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akiambatana na Viongozi wa TARURA, TANROAD na Kata ya Mburahati, Prof. Kitila amesema nyumba zinazopitiwa na barabara hiyo zitalipwa fidia ili Wananchi wahame kupisha mradi huo utakaopunguza foleni katika baadhi ya barabara kubwa.
“Fedha za mradi wa DMDP zitakazotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara hazihusishi fidia hivyo ili huu ujenzi ufanyike, itafanywa tathimini Sisi tutatafuta fedha za kuwafidia Wananchi ili mradi huu utekelezwe” Prof. Kitila Mkumbo.
Amesema uongozi wa Mburahati ulikuwa na madai mengi ya barabara lakini wametakiwa kuchagua kipaumbele ndiyo wakachagua barabara hiyo itakayoungana na Barabara ya Kawawa.
“Barabara hii ya Barafu – Darajani kuanzia wiki ijayo watakuja wataalam kwaajili ya kufanya tathimini ili malipo ya fidia yafanyike ujenzi uendelee” Prof. Kitila Mkumbo
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo ambaye ndiye Diwani wa Kata ya Mburahati amesema licha ya uwepo wa mvua Prof. Kitila amefika na kuona changamoto ya miundombinu inayowaka ili Wananchi.
Amesema kwa maendeleo yanayofanyika hakuna shaka kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kupendwa na Wananchi.
Miongoni mwa barabara zilizopitiwa kwenye ziara hiyo ni barabara ya Kagera – First Inn kwenda madoto na barabara ya
Tegemeo lami ambayo nayo itajengwa kwa kiwango cha lami.