Ukiwa ni mwendelezo wa Ziara za Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda kuwashukuru na kuwasikiliza Walipakodi mbalimbali ameonya uwepo wa wafanyabiasha wasiokuwa waaminifu wanaotengeneza pombe Bandia na kuweka Stika za TRA za kughushi.

Akiwa mkoani Manyara Kamishna Mkuu Mwenda amesema kughushi Stika za TRA ni makosa kisheria hivyo watawasaka wote wanaozalisha vinywaji changamshi Bandia ili wachukuliwe hatua za kisheria maana uzalishaji huo unaenda sambamba na matumizi ya Stika Bandia ili kuwaaminisha watumiaji.

Kamishna Mkuu Mwenda akiwa katika mkutano na wafanyabiasha mkoani Manyara amesema licha ya kukwepa kulipa kodi wazalishaji hao wa Pombe Bandia wanahatarisha usalama wa afya za watanzania kutokana na vinywaji vyao kutokuwa na viwango.

Kabla ya mkutano huo na wafanyabiasha CG Mwenda alitembelea kiwanda cha MAT cha mkoani Manyara kinachozalisha Pombe Kali maarufu kama Vinywaji changamshi na kumpongeza mmiliki wa kiwanda hicho Bw. David Mulokozi kwa kuwa Mlipakodi mzuri anayezingatia sheria.

Amesema wazalishaji wasiokuwa waaminifu wanaokiuka sharia za Nchi wamekuwa wakiwanyonya wenzao kwa kushusha bei na kuwafanya washindwe kushindana sokoni.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho cha MAT kinachozalisha Pombe Kali maarufu kama Vinywaji changamshi Bw. David Mulokozi amesema wataendeleza ubora na kusimamia sheria za TRA katika ulipaji wa kodi. 

About Author

Bongo News

1 Comment

    After research a few of the weblog posts on your website now, and I truly like your way of blogging. I bookmarked it to my bookmark website listing and shall be checking back soon. Pls take a look at my web page as effectively and let me know what you think.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *