Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amezindua zoezi la mafunzo na uibuaji wa miradi yenye mvuto wa ubia(PPPs) linaloendeshwa na kituo cha Ubia(PPPC) Tanzania.

Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimetoa mafunzo hayo ya uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri zake ambapo wataalam 42 wamepatiwa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo,yanayoratibiwa na wakufunzi Dr. Bravious Kahyoza na Michael Kihanga yana malengo muhimu ya Kuelewa dhana ya PPP na kuibua miradi yenye sifa ya utekelezwaji wa ubia, Kuandaa maandiko dhana (Project Concept Notes) pamoja na Kuandaa matangazo ya miradi kwa wawekezaji
Kutumia teknolojia ya GIS katika uwekaji wa miradi kwenye ramani za Halmashauri
Akifungua mafunzo hayo Mrindoko ameeleze kuwa mkoa wa Katavi ni mkoa wenye fursa lukuki za kiuwekezaji ambazo zina mvuto wa ubia.

Mrindoko amezitaja fursa hizo kuwa ni kwenye sekta ya mazao ya misitu kama ufugaji wa nyuki, utalii unaochagizwa na mbuga ya Katavi, uvuvi, usafirishaji na sekta ya kilimo.
Aidha, Mrindoko amempongeza, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyoimarisha uchumi. Amesema kwenye kipindi cha miaka minne, Rais Samia ametoa zaidi ya Shilingi Trillion 1.56 kwa ajili ya shughuli za maendeleo mkoani hapo.
Amesema fedha hizo zimesaidia kuimarisha sekta ya nishati ambapo zaidi ya 80% maeneo ya mjini yanapata umeme na 70% vijijini. Vilevile huduma za afya na miudombinu ya usafirishaji imeimarishwa.

Mrindoka amesema kuwa hatua hizi za uwekezaji kwenye miundombinu zitakuwa muhimu kwenye miradi ya PPP mkoani Katavi.
Kwa upande mwingine, Mrindoko amempongeza Rais Samia kwa kuanzisha kituo cha ubia(PPPC) na kuitaja hatua hiyo kama hatua ya kijasiri.
Mrindoko amesema kazi inayofanywa na kituo cha ubia chini ya Ndg. David Kafulila ni ya mfano kwani sasa dhana ya ubia inaanza kueleweka nchini.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo, Albert Msovela amesema mafunzo hayo yatakuwa na msaada mkubwa wa mkoa wa Katavi na kusisitiza kuwa mkoa uko tayari kushirikiana na PPPC kwenye shughuli za ubia.
PPPC inaendelea kutoa mafunzo katika mikoa 13 nchini kwa ajili ya uibuaji wa miradi ya PPP kwa maendeleo ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi hili.
1 Comment
Thanks for another fantastic article. Where else may anyone get that type of info in such a perfect way of
writing? I have a presentation next week, and I am on the search for such information.