KITAIFA

WAZIRI JAFO ATAKA TAFITI MABADILIKO YA TABIA NCHI, ILI KULINDA MAZINGIRA

WAZIRI JAFO ATAKA TAFITI MABADILIKO YA TABIA NCHI, ILI KULINDA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa watafiti kufanya tafiti zitakazosaidia kupata ufumbuzi wa changamoto za kimazingira hususan mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa rai hiyo wakati akizindua Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Tanzania imenufaika na zaidi ya shilingi bilioni 9 zilizotolewa na Serikali ya Norway kupitia Shirika la Maendeleo la NORAD katika makubaliano yaliyosainiwa na Serikali hizo mbili kwa ajili ya kufanya utafiti huo.

Waziri Jafo amesema kuwa uchumi unaweza ukaathirika kutokana na changamoto za kimazingira ambapo jamii hushindwa kufanya shughuli za kujipatia kipato ikiwemo kilimo na ufugaji kutokana na ukame.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo watafiti wanatarajiwa kutoa majawabu kuhusu sekta gani itasaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Maeneo haya tuna kazi kubwa ya kujua ni tafiti zipi kwa mfano kama ni kilimo gani kinaweza kufanyika katika maeneo yanayokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, ninyi watafiti mna jukumu kubwa la kutusaidia katika hili,” amesema.

Ameishukuru Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kusema kuwa hayo ni matunda ya diplomasia ya Mwanamazingira namba moja Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Niwapongeze COSTECH na Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Tanzania kwa upande wa research (utafiti) kwasababu tuna changamoto kubwa za athari za mabadiliko ya tabianchi na ndio maana tulijiwekea malengo ya kupungunguza emission ifikapo kwa asilimia 30 hadi 35,” amesema.

Kwa upande wao Mwenyekiti wa Bodi ya COSTECH Prof. Makenya Maboko pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungua wamesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na ushirkiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Wameshukuru Serikali ya Norway kupitia NORAD na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitaleta tija katika hatua ya utafiti
Kufanya utafiti

About Author

Bongo News

3 Comments

    he desires a new relationship but resists opening himself up to the possibility of getting hurt again.In therapy,ラブドール エロ

    I appreciate, cause I found just what I was looking for. You’ve ended my 4 day long hunt! God Bless you man. Have a nice day. Bye

    it’s still a fun secular celebration.セクシーコスプレThe offbeat custom is the legacy of a 1974 marketing campaign wherein the fast-food chain touted fried chicken as a traditional American yuletide feast.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *