KITAIFA

WAZIRI MAKAMBA AKERWA NA FITINA NDANI YA CCM, ASEMA 2025 FOMU NI MOJA TU KWA RAIS SAMIA

WAZIRI MAKAMBA AKERWA NA FITINA NDANI YA CCM, ASEMA 2025 FOMU NI MOJA TU KWA RAIS SAMIA

Raisa Said,Bumbuli
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Bumbuli  January Makamba Amesema    kwenye Chama Cha Mapinduzi CCM  kumekuwa na mambo ya kufitiniana hasa pale Rais aliyepo madarakani anapotakiwa kuendelea na muhula wa pili.

Hayo ameyasema  kijijini kwao Mahezangulu Halmashauri ya  Bumbuli Mkoani Tanga  wakati wa Maulidi ya 40 inayofanyika kila Mwaka siku ya idd pili kijijini hapo  ya kuwaombea ndugu zao waliotangulia mbele za haki.

Makamba alisema chanzo kikubwa Cha kufitiniana ni wanapokuwa na Rais anae stahili  kuendelea  kuongoza Kipindi Cha pili nakwamba katika nyakati hizo watu ndani ya chama hicho  hufitiana hasa.

” Kama vile ada kwenye ccm watu wakitaka kufitiniana wanasema unamuona yule  bwana hataki huyu aendelee,unamuona yule bwana ana njamanjama ili huyu aonekane hafai,unamuona yule bwana anatega huyu ashindwe  ndo tulivyo “Alisisitiza Makamba  nakuongeza kuwa wakati siku zote huamua” alieleza Makamba

” Ndugu zangu tuendelee kuombeana  fitina hizi zisiwe na mashiko kwenye  nchi yetu na kwenye Chama chetu ,nazitakoma siku ile sa kumi jioni mgombea wa kiti Cha Urais kupitia CCM atakapokuwa kachukua mtu  mmoja pekee kutoka ndani ya CCM ambaye ni Rais Samia” Alisema Makamba.

Waziri Makamba amesisitiza kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani mgombea pekee atayegombea nafasi hiyo ya kiti Cha Urais  ni  Rais Samia kama ilivyo utaratibu wa siku zote Wa chama hicho.

Waziri Makamba alisisitiza kuwa nchi ya Tanzania imebarikiwa kupata  Rais anaye ongoza  vizuri kwa busara  na hekima nakwamba hiyo imepelekea nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu .

Hata hivyo alitumia jukwaa hilo  kueleza hatua ya kuongozwa na Rais Samia kuwa ni baraka kwa  kuwa ni kiongozi mwenye busara na hekima  mambo yanayochagiza Maendeleo ,amani na utulivu wa nchi.

About Author

Bongo News

1 Comment

    The next morning is my final morning. I take a final naked swim and pack up all the clothesえろ 人形 I didn’t wear. My shuttle to the airport is shared with a strikingly attractive young couple.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *