KITAIFA

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA TASAF KUWA SHIRIKISHI ILIKUWAGUSA WALENGWA HALISI WA UMASIKINI

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA TASAF KUWA SHIRIKISHI ILIKUWAGUSA WALENGWA HALISI WA UMASIKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George ameutaka Uongozi wa  Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii  (TASAF)  kuwa shirikishi  katika mchakato wa
kuwabaini walengwa halisi ambao ni maskini huku akiwasisitiza
kuwatumia  Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mchakato huo. 
Imeelezwa kuwa licha ya TASAF kufanya kazi yake nzuri ya kukwamua
kaya masikini kwenye lindi la umasikini lakini kumekuwa na minong’ono
kuwa wanaopata ruzuku hiyo sio walengwa halisi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi hao iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.


Kauli hiyo ameitoa leo Alhamisi Julai 13, 2023  wakati wa ziara yake ya
kikazi  Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na
Watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Amesema Maafisa Maendeleo hao wa Jamii ni watu muhimu sana
katika zoezi hilo  kwa vile wapo katika ngazi ya Kata  pamoja na ngazi
ya Kijiji, hivyo wanawajua walengwa halisi.

Sehemu ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.


‘’Watumieni hawa kwani licha ya kuishi na walengwa hawa lakini pia
Maafisa hawa wamekuwa wakishiriki katika vikao vya Madiwani’
amesisitiza Mhe Simbachawene.
Amefafanua kuwa, TASAF msingi wake ni  mpango shirikishi wa
kuondoa umasikini hivyo, inatakiwa kuwashirikisha viongozi katika
maeneo husika ili iweze kutimiza azma ya kuanzishwa kwake. 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene baadhi ya ofisi za TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi hao iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa TASAF jijini Dar es Salaam.  


Hata hivyo, Mhe.Simbachawene amesema TASAF bado inahitajika sana
kwa vile bila uwepo wake, umaskini ungekuwa umeongezeka kwa kiasi
kikubwa sana na kusisitiza kuwa itaendelea kuzikwamua kaya zilizoko
kwenye umasikini uliokithiri.
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Memejimenti ya Utumishi wa Umma,
Mhe.Ridhiwani Kikwete amewapongeza watumishi wa TASAF kwa kazi
nzuri wanayoifanya huku akisisitiza kuwa TASAF imesaidia ongezeko la
wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa TASAF kumesaidia
kupunguza migogoro kwenye ngazi ya kaya baada ya wananchi wengi
maskini kujihusisha kwenye na uzalishaji mali.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao. Wa pili kulia waliokaa ni Naibu Waziri wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete na wa pili kushoto waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Shedrack Mziray.


Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray
amesema atatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na viongozi hao ikiwa
ni  pamoja na kuhakikisha walengwa wa ndio wanakuwa
wanufaika namba moja.
TASAF ilianzishwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tatu lengo likiwa ni
kuondoa umasikini uliokithiri kwa wananchi katika maeneo ya vijijini na
maeneo machache ya mjini kwa kuwashirikisha kwenye shughuli za
kiuchumi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *