KITAIFA

WAZIRI SIMBACHAWENE APONGEZA NGUVU ZA WANANCHI KUJENGA SHULE YA KISASA LUMUMA

WAZIRI SIMBACHAWENE APONGEZA NGUVU ZA WANANCHI KUJENGA SHULE YA KISASA LUMUMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Walimu wa  Shule ya Sekondari Lumuma Green ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Lumuma katika Jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma kabla ya  mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Wananchi wa Kata ya  Lumuma kwa kazi kubwa waliyoifanya ya  kujenga  Shule ya Sekondari ya Lumuma Green kwa nguvu zao wenyewe ambayo ina wanafunzi 106  wa kidato cha kwanza kutoka vijiji vitatu vinavyounda Kata hiyo.

Ametoa Pongezi hizo wakati akizungumza na  Wananchi  kwa nyakati tofauti katika vijiji  vya Lufusi, Kitati na  Lumuma Mafene  Kata ya Lumuma kupitia mikutano ya hadhara anayoendelea kuifanya katika Vijiji vya Jimbo la Kibakwe,  ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na wananchi  wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Lumuma  ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe

Amesema amefurahishwa na uthubutu na utayari uliooneshwa na wananchi wa Kata hiyo kwa kukubali kuunganisha nguvu zao kwa  pamoja katika kukamilisha shule hiyo yenye majengo ya kisasa.

Amesema Serikali inavutiwa na uongozi wenye maono na mtazamo wa kimapinduzi kwa kuanza kusaidia pale nguvu za wananchi zilipoishia ili kuistawisha jamii hiyo.

Amemtaja Diwani wa Kata hiyo Mhe. Jocktan Cheligah kama Kiongozi mwenye uthubutu na mbunifu ambaye amedhamiria kuhakikisha shule  hiyo inajengwa ili wanafunzi wa vijiji hivyo wanapata elimu katika mazingira rafiki.

Sehemu ya wananchi wa Kata ya Lumuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene  wakati wa  mkutano wa hadhara katika Jimbo la Kibakwe ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe

Kufuatia hatua hiyo Mhe. Simbachawene ameahidi kusaidia kujenga nyumba pacha tatu kwa ajili ya kuwasaidia walimu ambao wanaishi mbali na eneo la shule.

Amesema akiwa ndiye Mbunge wa jimbo lao la Kibakwe, anahitaji wananchi wanaoonesha njia ili Serikali iweze kusaidia kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

‘’Kwa kujenga shule hii, mimi binafsi mmenitia moyo, hivyo naomba niwaahidi kuwa nitahakikisha hadi kufika mwakani tunakuwa na majengo mengi zaidi ili watoto wetu wasome katika mazingira bora’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene

Amefafanua kuwa, nguvu za wananchi zinahitajika ili kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kwani Serikali ina vipaumbele vingi hivyo bila wananchi wenyewe kuanza kubuni miradi hiyo huwa ngumu kuitekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Baadhi ya muonekano wa majengo ya shule ya Sekondari Lumuma Green ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Lumuma katika Jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma ambapo amewapongeza wananchi hao kwa kazi kubwa waliyofanya. 

Katika hatu nyingine Mhe. Simbachawene ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa zahanati ulioibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Lufusi na kuahidi kuwa ataisaidia katika ukamilishaji wa Zahanti hiyo kwa wakati.

‘’Naomba niwaahidi kuwa, kuptia mfuko wa Jimbo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa tutahakikisha fedha zinapatikana ili kusaidia katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa zahanati hiyo mliyoanza.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. George Fuime ameahidi kutenga fedha za kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo kwa nia ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wananchi wa Kata hiyo.

“Tutahakikisha fedha zinatengwa kwa ajili ya kuunga nguvu za wananchi katika masuala ya maendeleo yaliyobuniwa na wananchi wenyewe, amesema Mhe. Fuime.

Naye Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Jocktan Cheligah ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Simbachawene kwa utayari wake wa kukubali kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa wananchi anaowaongoza.

About Author

Bongo News

1 Comment

    com is leading the way in doll realism,リアル ドールand my experience with them has been exceptional.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *