KITAIFA

WAZIRI SIMBACHAWENE AZIASA NCHI ZA AFRIKA KUWA NJIA YA PAMOJA YA KUPAMBANA NA TATIZO LA RUSHWA

WAZIRI SIMBACHAWENE AZIASA NCHI ZA AFRIKA KUWA NJIA YA PAMOJA YA KUPAMBANA NA TATIZO LA RUSHWA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifungua Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema rushwa Barani
Afrika ni tatizo linalohitaji njia ya pamoja ya kupambana nalo kwani utoaji
na upokeaji rushwa unabadilika kulingana na msukumo wa maendeleo
ya sayansi na teknolojia pamoja maisha ya watu kadiri yanavyobadilika. 
Imeelezwa kuwa ni muda muafaka sasa kwa nchi za Afrika kuwa na
sheria zinazofanana katika kushughulikia tatizo hilo, hali itakayopelekea
kutokomeza kabisa tatizo la rushwa. 

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Akizungumza  kwenye  ufunguzi wa Kongamano la kujadili namna bora
ya kupambana na rushwa, ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku
ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka
Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa
Tanzania, jijini Arusha, Mhe. Simbachwene amesema mbinu za
kupambana na rushwa ni lazima kubadilika kulingana na maendeleo ya
sayansi na teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP Salum Hamduni akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufungua  Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Amesema kongamano hilo ikiwezekana litoke na maazimio ya pamoja
yatakayopelekea nchi zote za Afrika kuwa na sheria zinazofanana ili
watuhumiwa wa rushwa wa nchi hizo wajue kabisa kuwa
watawajibishwa kupitia sheria hizo. 
Amesema kuwa tatizo la rushwa Barani Afrika ni kubwa na linahitaji
sauti ya pamoja huku akitolea mfano wa rushwa kwenye suala la utoaji
wa elimu na kusema kuwa kama hatua za pamoja hazitachukuliwa
kutapelekea kuwa na vijana wahitimu ambao ni zao la rushwa.
Kufuatia hatua hiyo amezihimiza nchi za Afrika kutumia Kongamano hilo
kujadili namna bora ya kutumia sayansi na teknolojia katika utoaji
huduma utakaowezesha kuzuia watu kukutana ana kwa ana huku
akisisitiza mifumo hiyo iwekwe ili kudhibiti rushwa katika sekta
mbalimbali.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) CP. Salum Hamduni amesema Kongamano hilo,
mbali ya kuwakutanisha Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa
Barani Afrika pia limewakutanisha Wadau wa kupambana na rushwa wa
ndani na nje ya nchi, hivyo Kongamano hilo ni darasa huru la kujifunza
na kupata uzoefu wa kupambana na rushwa kwa nchi moja moja na
Afrika kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa rushwa inatokomezwa kabisa.
Ameongeza kuwa Kongamano hilo pamoja na kujadili mada mbalimbali
za kupambana na rushwa Barani Afrika pia watajadili mbinu mbalimbali
za kupambana na tatizo hilo kidigitali ikizingatiwa kuwa utoaji wa rushwa
kwa sasa unafanyika kidigitali. 

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia tamati kesho Julai 11, 2023
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia
Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *