KITAIFA

WIZARA YA AFYA YAZINDUA UTAFITI WA KITAIFA WA VIASHIRIA VYA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA (STEPS SURVEY 2023)

WIZARA YA AFYA YAZINDUA UTAFITI WA KITAIFA WA VIASHIRIA VYA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA (STEPS SURVEY 2023)

Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambaye ndiye Mtafiti mkuu akikabidhiwa vifaa kwa ajili ya utafiti huo ambao unatarajiwa kuanza mapema mwezi Agosti mwaka huu na itafanyika mikoa yote Tanzania bara na zanzibar ikihusisha watu wenye umri  kati ya miaka 18 hadi 69.

Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) yanachangia takribani 33% ya vifo vyote nchini huku  kwa takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo  milioni 41 sawa na 71% ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo milioni 57 kwa mwaka 2016 duniani.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ally Mazrui wakati wa Uzinduzi wa Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza (STEPS SURVEY 2023) uliofanyika kwenye ukumbi wa Tawimu Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ally Mazrui akiongea wakati wa Uzinduzi wa Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza (STEPS SURVEY 2023) uliofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Mhe. Mazrui amesema takwimu zinaonesha kuwa magonjwa hayo yameongezeka mara 5 hadi 9 zaidi kati ya miaka ya 80 ambapo 1% tu ya watanzania walikuwa na tatizo la kisukari na 5%  walikuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu  wakati kwa sasa tatizo la kisukari limefikia asilimia 9 na tatizo la shinikizo la juu la damu limeongezeka na kufikia asilimia 25.

“Takwimu hizo zote kutoka katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya nchini zinaonesha ongezeko kubwa sana la magonjwa hayo ambapo katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, Magonjwa Yasiyoambukiza ambayo yalisababisha wagonjwa wengi kuhudhuria vituo vya huduma za afya ni pamoja na shinikizo la juu la damu wagonjwa 1,456,881 sawa na asilimia 49 ukilinganisha na asilimia 34  kipindi kama hicho mwaka 2021/2022 ,Kisukari wagonjwa 713,057 sawa na asilimia 24,  magonjwa ya mfumo wa hewa wagonjwa 386,018 sawa na asilimia 13 ikilinganishwa na asilimia 10 kwa kipindi  kama hicho mwaka 2021/2022.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu  amesema katika familia tunapaswa kubadili mtindo wa maisha, ulaji wetu, kufanya mazoezi na pia kupunguza msongo wa mawazo kwani katika magponjwa yasiyoambukiza kuna magonjwa ya akili ambayo huwa yana hatua mbalimbali.

Aidha, amesema katika kukabiliana na  ongezeko la magonjwa hayo, Serikali  inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutekeleza mkakati wa Kitaifa  wa kukabiliana na magonjwa hayo nchini kwa kutoa elimu  kwa jamii kuhusu namna bora  ya kujikinga na magonjwa hayo pamoja na kuimarisha  mifumo ya utoaji huduma za afya nchini kwa kufikisha huduma za uchunguzi wa awali na matibabu kuanzia ngazi  ya afya ya msingi.

“Kufuatia mwenendo na hali ya magonjwa haya nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na WHO inakwenda kufanya utafiti wa Kitaifa utakaobaini  hali halisi ya mwenendo wa viashiria hatarishi na magonjwa yasiyoambukiza. Utafiti huu utakuwa ni wa pili   baada ya ule wa kwanza  uliofanyika mwaka 2011 upande wa Zanzibar na mwaka 2012 kwa upande wa Tanzania Bara”. Aliongeza.

Amesema utafiti huo unatarajiwa kuanza tarehe 14 Agosti,2023 na  unatarajia kuifikia mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar ukihusisha watu wenye umri kati  ya miaka 18 hadi 69 na utafiti huo unapaswa kufanyika kila baada ya miaka minne hadi mitano.

“Utafiti huu ni muhimu sana hasa katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza na takwimu hizo za kisayansi zitaonesha juu ya ukubwa wa viashiria vya magonjwa hayo nchini ambavyo vinaweza kutumika katika kuandaa mikakati ya kudhibiti magonjwa hayo nchini” Alisisitiza

Hata hivyo amewakumbusha  watafiti wote watakaoshiriki katika zoezi hilo kuhakikisha ubora wa takwimu zitakazokusanywa  na kuzingatia maadili wakati wote wa utekelezaji wa utafiti huo.

Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amesema nchi inakabiliwa na majanga mawili ya  magonjwa ya kuambukiza ikiwemo TB, UKIMWI, Malaria lakini na magonjwa yasiyoambukiza  ambapo kwa sasa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na kuongezea mzigo mkubwa wa bajeti ya Serikali hususani Wizara ya Afya na gharama kwa familia.

Amesema kumekua na vifo vya kabla ya wakati vikitokea ambavyo vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza na hata ubora wa maisha imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya magonjwa hayo licha ya kuwa na dawa za kutibu magonjwa hayo na ndio maana wanajikita katika utafiti.

“Kipaumbele chetu ni kukinga na kwa wale ambao tayari wamegundulika tunawapa matibabu na ndio maana  tumeimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya nchini kwa kufikisha huduma za uchunguzi wa awali na matibabu kuanzia ngazi ya afya ya msingi ambapo ugatuzi wa huduma za matibabu na uchunguzi wa awali wa magonjwa haya kufanyika kuanzia ngazi ya vituo vya afya na zahanati”.

Prof. Nagu amesem utafiti huo utasaidia  kujua ukubwa wa tatizo na kuwawezesha kujipanga katika kugawa rasilimali kwa maana watakuwa wanajua tatizo na hivyo kutambua tatizo lilipo na kutibu mapema.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya kutoka OR-TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera amesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia  katika sekta ya afya hususan katika ngazi ya msingi ili kuweza kupunguza changamoto za matibabu kwani wananchi wengi zaidi ya 90% wanaanzia kupata  huduma za afya ngazi za msingi na pia  Serikali imeweza kuboresha miundombinu ya kutolea huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Dkt. Mahera amesisitiza Mikoa, Halmashauri na vituo vya afya kuwa na mipango ya bajeti sahihi ambayo inalenga mahitaji sahihi ya magonjwa yasiyoambukiza kwani kuwa na takwimu sahihi itasaidia kuweka mipango mizuri ya kupambana na adui maradhi hususani magonjwa yasiyoambukiza.

About Author

Bongo News

11 Comments

    Thus the data indicates that spaying and neutering actually increases the severity of the problem behaviors that they are intended to solve.ラブドール 中古A new study by a team of investigators headed by David Vajányi at the University of Veterinary Medicine and Pharmacy in Košice,

    ランジェリー ショップwhich at 181 square miles is smaller than Chicago,could soon turn into one of the world’s biggest ski destinations.

    The realism is incredible,美人 セックスwith lifelike skin texture and finely crafted facial features.

    (Bonus: It also comes in six other colors,from a bridal white to something blue for your wedding night or honeymoon vacation.sexy velma

    ‘Regardless of gender, age or sexuality, everyone has some sexual shame,’ ラブドール 女性 用says Todd Baratz, a certified sex therapist and couples psychotherapist.

    The choice between silicone and TPE is pivotal,ドール オナニー each material bringing its unique qualities to the forefront.

    The familiarity of having a ‘companion’ can be comforting, particularly for jydollthose suffering from conditions like dementia, where a doll can provide a semblance of normalcy and emotional support.

    I feel this is one of the so much significant info for me.
    And i am satisfied reading your article. But want to remark on few common issues, The website
    style is perfect, the articles is really great :
    D. Good job, cheers

    If you tell someone “no” or disagree with them—and find what you receive in return are threats to harm you in some way,however small they may seem at the time,ダッチワイフ

    The way you presented [specific subtopic] was not only captivating but also deeply informative.I particularly enjoyed how you used engaging narratives and real-life examples to illustrate complex theoretical concepts,ラブドール

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *